Sura 79 An-Nazi'at, aya 1 – 14

  1. وَالنَّازِعَاتِ غَرْقًا

    Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu!

    79:1
  2. وَالنَّاشِطَاتِ نَشْطًا

    Na kwa wanao toa kwa upole!

    79:2
  3. وَالسَّابِحَاتِ سَبْحًا

    Na wanao ogelea!

    79:3
  4. فَالسَّابِقَاتِ سَبْقًا

    Wakishindana mbio!

    79:4
  5. فَالْمُدَبِّرَاتِ أَمْرًا

    Wakidabiri mambo.

    79:5
  6. يَوْمَ تَرْجُفُ الرَّاجِفَةُ

    Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka!

    79:6
  7. تَتْبَعُهَا الرَّادِفَةُ

    Kifuate cha kufuatia.

    79:7
  8. قُلُوبٌ يَوْمَئِذٍ وَاجِفَةٌ

    Siku hiyo nyoyo zitapiga piga!

    79:8
  9. أَبْصَارُهَا خَاشِعَةٌ

    Macho yatainama chini!

    79:9
  10. يَقُولُونَ أَإِنَّا لَمَرْدُودُونَ فِي الْحَافِرَةِ

    Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza?

    79:10
  11. أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا نَخِرَةً

    Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa?

    79:11
  12. قَالُوا تِلْكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ

    Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara!

    79:12
  13. فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ

    Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu,

    79:13
  14. فَإِذَا هُمْ بِالسَّاهِرَةِ

    Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano!

    79:14

Tafsiri: Ali Muhsin al-Barwani